Home KITAIFA WAKAZI WA BONDE LA MAJI LA MTO MAKATA KUJENGEWA SKIMU YA KIMBANDE

WAKAZI WA BONDE LA MAJI LA MTO MAKATA KUJENGEWA SKIMU YA KIMBANDE

Nyasa

WAKAZI wanaoishi Kata za Kilosa na Mbambabay, na Kijiji cha Ndesule kujengewa skimu ya umwagiliaji itakayoitwa Kimbande (jina linalotokana na maeneo hayo matatu).

Hayo yamesemwa na Waziri wa Kilimo,Hussein Bashe Septemba, 20 2024, Wilayani Nyasa ambaye aliambatana, Mbunge wa Nyasa,Mhandisi Stella Manyanya na Mkuu wa Wilaya ya Nyasa,Peres Magiri, ambao walitaka kumuonesha uhitaji wa skimu hiyo kwa wakazi hao.

“Nailekeza Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kuanza ujenzi wa skimu ya Kimbande ambayo Ina ekari 750 za kilimo cha mpunga. Ujenzi uwe na awamu mbili, kutengenezwe kingo za maji ili yabaki kwenye mto; na pili kuwe na sehemu ya kukusanya maji ili yawe juu kama mabwawa,” amesema Waziri Bashe.

Ameomba wakulima na wafugaji waliopo pembezoni mwa mto Makata kutoa ushirikiano na kupisha ujenzi wa skimu pale kazi itakapoanza.

Waziri Bashe yupo katika ziara ya kikazi katika kuleta maendeleo kwa wakazi wa Mkoa wa Ruvuma kuanzia 17 hadi 24 Septemba 2024.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here