Home KITAIFA ”MKOA WA TABORA TUMEPIGA VITA MAFUNDI UMEME VISHOKA”-RAS TABORA

”MKOA WA TABORA TUMEPIGA VITA MAFUNDI UMEME VISHOKA”-RAS TABORA

Tabora

KATIBU Tawala wa Mkoa wa Tabora, Dk. John Mboya, akifungua semina ya siku moja kwa mafundi umeme wa mkoa huo, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Paul Matiko Chacha, leo Septemba,17 2024,amewasihi mafundi umeme wote mkoani humo kuhakikisha wanakuwa na leseni za ufungaji mifumo ya umeme zinazotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kwa mujibu wa Kifungu cha. 8 (h) cha Sheria ya Umeme,Sura Na. 131.

Katibu Tawala Mkoa wa Tabora, Dk. John Mboya,

“Kuanzia leo, mkoa wa Tabora tumepiga vita mafundi vishoka, na ni imani yangu kwamba baada ya semina hii kila asiye na leseni ataomba leseni ili afanye kazi kwa uhalali, ninawasihi sana tusipoteze fursa hii kwani mkoa wetu una miradi mingi ambayo ni fursa kwa mafundi umeme na kuanzia sasa vishoka wote hawatapewa kazi mpaka pale watakapokuwa na leseni ya EWURA,” am3sema.

Meneja wa EWURA Kanda ya Magharibi, Mhandisi Walter Christopher

Meneja wa EWURA Kanda ya Magharibi, Mhandisi Walter Christopher, amesema semina hiyo iliyowashirikisha mafundi umeme na wadau zaidi ya 150, ililenga kuwajengea uwezo wataalam na wadau hao kuhusu sheria, kanuni, miongozo na utaratibu wa utendaji kwenye shughuli za ufungaji wa mifumo ya umeme.

Wadau wengine walioshiriki semina hiyo ni Wakala wa Usimamizi wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (TANESCO), Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Wakala wa Majengo (TBA) na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA).

Mafundi umeme wanaweza kuomba leseni kupitia mfumo wa LOIS unaopatikana kwenye tovuti ya EWURA www.ewura. go.tz na kupakua fomu ya kukamilisha ufungaji mifumo ya umeme katika tovuti hiyo hiyo au kuwasiliana na EWURA kwa simu 0800110030, mitandao ya kijamii au barua pepe; info@ewura.go.tz.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here