📌 Mitungi ya Gesi 400,000 yapewa Ruzuku
📌 Dkt. Biteko Asisitiza Nishati Safi ya Kupikia kwa Wote
Dodoma
NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko amesema Serikali inafanya kila jitihada kuhakikisha kunakuwa na unafuu katika upatikanaji wa bidhaa za nishati safi ya kupikia ikiwemo mitungi ya gesi ili kumwezesha kila mwananchi kutumia nishati iliyo safi na salama.
Dk. Biteko amesema hayo Septemba,13 2024 jijini Dodoma wakati wa hafla ya Kusainiwa mikataba ya ushirikiano ya utekelezaji wa Nishati Safi ya Kupikia yenye thamani ya shilingi bilioni 50.98 kati ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na taasisi sita ambazo ni Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Jeshi la Magereza (TPS) na Wasambazaji wa Gesi ya kupikia, hafla ambayo ilienda sambamba na uzinduzi wa jengo la REA.