Home KITAIFA WAZIRI BASHE AGAWA TREKTA 400, PIKIPIKI 1000 NA BAISKELI 2500 KWA WAKULIMA

WAZIRI BASHE AGAWA TREKTA 400, PIKIPIKI 1000 NA BAISKELI 2500 KWA WAKULIMA

Tabora

WAKULIMA wa Zao la Pamba nchini wanatarajia kunufaika na zana za kilimo kufuatia ugawaji wa trekta 400, pikipiki 1000 na baiskeli 2500, boza 58 kwa ajili ya viuatilifu vya dawa na mbolea hai lita 3000.

Zana hizo zimekabidhiwa na Waziri Kilimo, Hussein Bashe kufuatia ziara yake ya kikazi katika Wilaya ya Igunga, Mkoa wa Tabora Septemba,11 2024.

“Serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan inalenga kuendelea kuwekeza kwa wakulima ili wazalishe mazao kwa tija. Na tutaendelea na mpango wa kuchimba mabwawa ili waanze pia kuvuna maji ya mvua na kuwa na Kilimo cha umwagiliaji,” amesema Waziri Bashe.

Ameongeza kuwa ni vyema wakulima hao kutumia ipasavyo fursa na nyenzo hizo za kilimo na kupuuza baadhi ya wanasiasa.

“Serikali hii haiwezi kutoa dawa feki, mbegu feki na wanunuzi feki kwa wakulima. Siasa zinaleta uchochezi kwa wakulima zinaharibu maisha ya watu na hilo sitoruhusu huo mchezo kwenye Sekta ninayosimamia,” amesema Waziri Bashe.

“Hatuwezi kuwa na Taifa linatukana watu, linatukana Serikali tunakaa kimya. Watu walikuwa na mateso walikopwa, pamba zilidoda. Miaka miwili tumetoa ruzuku ya mbolea bure na tutaendelea kufanya hivyo na tutaendelea kununua mazao,”amefafanua Pia ameeleza nia ya wizara kuweka kituo cha ununuzi wa nafaka Wilayani Igunga.

Aidha, Waziri Bashe ametumia fursa hiyo kueleza mipango ya Serikali ya kujenga mabwawa na miundombinu ya umwagiliaji ya kutosha Igunga kwa kuwa kitakwimu ni ya kwanza au ya pili, hivyo ni lazima kuwa na uzalishaji wa uhakika kwa kilimo cha umwagiliaji cha Pamba.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here