Home KIMATAIFA RAIS SAMIA AKUTANA NA RAIS XI JINPING WA CHINA. 

RAIS SAMIA AKUTANA NA RAIS XI JINPING WA CHINA. 

CHina

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan amefanya mkutano  na Rais wa China, Xi Jinping pamoja na ujumbe wake mapema leo katika ukumbi wa The Great Hall of the People jijini Beijing.

Rais Samia  amefanikiwa kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia ya Tanzania na nchi muhimu duniani ikiwepo China tangu alipoingia madarakani Mwaka 2021. 

Kwa Mwaka huu wa 2024 Rais Samia na Xi Jinping wamejadiliana kuimarisha  uhusiano wetu mzuri uliodumu zaidi ya miaka 60.

Vilevile baada ya kikao hicho Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk. Samia Suluhu Hassan, Rais Jamhuri ya Watu wa China, Xi Jinping pamoja na Rais wa Zambia Hakainde Hichilema walishuhudia uwekaji saini wa hati ya makubaliano ya kuboresha reli ya TAZARA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here