📌 Ahimiza kuchagua viongozi watakaowaunganisha
📌Awapongeza NMB kwa maendeleo nchini
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko ametoa rai kwa Watanzania kuchagua Viongozi wa Serikali za Mitaa wanaofaa kwa maendeleo ya Taifa.
Dk. Biteko amesema hayo leo Agosti 31, 2024 wakati wa NMB Bunge bonanza iliyofanyika katika viwanja vya Shule ya John Merlin jijini Dodoma.