Home AFYA MUHIMBILI MLOGANZILA KUENDELEA KUTOA MATIBABU YA UPANDIKIZAJI WA NYONGA NA MAGOTI

MUHIMBILI MLOGANZILA KUENDELEA KUTOA MATIBABU YA UPANDIKIZAJI WA NYONGA NA MAGOTI

Dar es Salaam

MKURUGENZI Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili(MNH), Profesa Mohamed Janabi amesema hospitali hiyo itaendelea kutoa matibabu ya ubingwa bobezi ikiwemo upandikizaji wa nyonga na magoti hapa nchini kwa lengo la kupunguza usumbufu na gharama za kufuata matibabu hayo nje ya nchi.

Profesa.Janabi ameyasema hayo leo Agosti, 25 2024 Jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu kuanza rasmi kwa kambi maalum ya upandikizaji nyonga na magoti kwa kushirikiana na Daktari Bingwa wa nyonga na magoti mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 30 kutoka nchini India, Dk. Venuthuria Ram Mohan Reddy ambayo imeanza leo na itadumu kwa muda wa siku tano.

Ameongeza kuwa pamoja na kushirikiana na Dk. Venuthuria Ram Mohan Reddy wataalam wa ndani wana weledi na ujuzi wa kutosha katika eneo la upandikizaji wa nyonga na magoti, hivyo kinachofanyika sasa ni kuongeza maarifa zaidi ya namna matibabu haya yanavyofanyika duniani.

“Sio mara ya kwanza kwa kufanya matibabu haya katika hospitali yetu ya Muhimbili-Mloganzila, tumeshawafanyia wagonjwa takribani 173 na sasa wanaendelea vizuri, upasuaji huu wa upandikizaji wa nyonga na magoti ni salama hivyo hakuna sababu ya mtu kukaa na maumivu wakati suluhisho la matatizo lipo,” ameongeza Profesa Janabi.

Kwa upande wake Daktari Bingwa Mbobezi wa Upandikizaji wa Nyonga na Magoti Dk. Abubakar Hamis amesema kati ya wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa upandikizaji wa nyonga na magoti kwa kwengi wao imetokana na uzito ulipitiliza na umri mkubwa.

Naye Daktari Bingwa Bobezi wa Upasuaji wa Nyonga na Magoti Profesa Venuthuria Ram Mohan Reddy amebainisha kuwa katika kambi hii ya siku tano atatumia fursa hiyo kubadilishana uzoefu kati yake na wataalam wa hospitali hiyo.

Aidha, Mchezaji wa Zamani wa timu ya mpira wa miguu Tanzania, Mzee Sunday Manara ambaye alifanyiwa upasuaji wa upandikizaji wa nyonga miezi miwili iliyopita Muhimbili-Mloganzila amesema kwa sasa anaendelea vizuri na kuwasihi watanzania kujitokeza kupata huduma hizo kwakuwa hazina changamoto yoyote.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here