Home KITAIFA DCP NYAMBABE AKABIDHI BENDERA KWA ASKARI WA KIKE WANAOKWENDA KUSHIRIKI MAFUNZO YA...

DCP NYAMBABE AKABIDHI BENDERA KWA ASKARI WA KIKE WANAOKWENDA KUSHIRIKI MAFUNZO YA DUNIA NCHINI MAREKANI.

Dar es Salaam.

NAIBU Kamishna wa Polisi Kutoka kitengo cha Udhibiti Makosa yanayovuka Mipaka, DCP Daniel Nyambabe amewakabidhi askari wa kike Bendera ya Taifa kwa ajili ya Kwenda nchini Marekani kushiriki mafunzo kwa askari wa kike Duniani katika jimbo la Chicago Nchini humo kuanzia Septemba 01 hadi 05, Mwaka huu.

DCP Nyambabe akikabidhi bendera hiyo leo Agosti 26,2024 Makao Makuu Ndogo ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam amesema kwa askari hao wanakwenda kuhudhuria mafunzo hayo ya Dunia ambayo yanahusisha askari wa kike na wasimamizi wa sheria ambapo amewasisitiza kuzingatia mafunzo nchini Marekani.

Ameongeza kuwa Jeshi la Polisi linaamini kuwa mafunzo wanayokwenda kuyapata yataleta chachu ya mabadiliko ya kiutendaji ndani ya Jeshi la Polisi huku akibainisha kuwa Jeshi hilo linaamini kuwa washiriki hao ni kielelezo kizuri cha nchi ambapo amewataka kuwa na nidhamu kipindi chote cha mafunzo.

Aidha ameeleza kuwa kuwa ushiriki wa askari wa Jeshi la Polisi katika mafunzo hayo ya Dunia ni uwakilishi wa Nchi ambapo amewataka askari hao Kwenda kulinda na kutunza taswira nzuri ya nchi iliyojengwa kwa muda mrefu na waasisi wa nchi hii.

Pia DCP Nyambabe amewaomba maafisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali kutumia fursa ya mafunzo hayo kutengeneza mtandao wa mawasiliano ambayo yatasaidia katika mapambano dhidi ya uhalifu na kumjengea uwezo askari mmoja mmoja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here