Home KITAIFA RAIS DK.SAMIA APONGEZA USHIRIKI WA TAWA KIZIMKAZI

RAIS DK.SAMIA APONGEZA USHIRIKI WA TAWA KIZIMKAZI

Zanzibar

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amekabidhi cheti cha pongezi kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kutokana na ushiriki wake wa kipekee katika Tamasha la Tisa la Kizimkazi lililofanyika Kusini Unguja, Zanzibar kuazia tarehe 18-25 Agosti, 2024.

Cheti hicho cha pongezi kilipokelewa na Afisa Utalii Mustapha Buyogera katika hafla ya chakula cha usiku iliyofanyika Ikulu ndogo, Kizimkazi, Zanzibar.

Katika tamasha hilo, Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia TAWA limekuwa kivutio kikubwa kwa wananchi wengi na wadau mbalimbali wa utalii ambapo wageni walipata fursa ya kushuhudia wanyamapori hai waliopo katika bustani ya wanyamapori hai.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here