Home KITAIFA RAIS MWINYI: WEKEZENI KWENYE MAADILI YA VIJANA NA WATOTO

RAIS MWINYI: WEKEZENI KWENYE MAADILI YA VIJANA NA WATOTO

Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj. Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameinasihi jamii kuweka mkazo katika malezi ya vijana na watoto ili kuwanusuru na mmomonyoko wa maadili.

Alhaj. Dk. Mwinyi ameyasema hayo leo Agosti,23 2024, alipotoa salamu baada ya kushiriki katika sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Shuraa uliopo Magomeni, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Ameeleza kuwa kumekuwa na mmomonyoko mkubwa wa maadili na vitendo viovu vinavyosababishwa na vijana kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya na unywaji wa pombe uliokithiri.

Amewahimiza wazazi kuhakikisha vijana wanapata elimu ya dini kwa ajili ya kujitambua na kujiepusha na vitendo viovu.

Alhaj. Dk. Mwinyi ameongeza kuwa Zanzibar ilikuwa nchi yenye sifa katika kusimamia maadili, lakini yameporomoka kutokana na matumizi ya dawa za kulevya kwa kundi kubwa la vijana.

Aidha, amewahimiza viongozi wa dini kuendelea kuhubiri na kuwahimiza waumini kufuata misingi ya dini ili kuirejesha nchi katika maadili mema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here