Home KITAIFA SERIKALI INATHAMINI NA KUTAMBUA MCHANGO WA MADEREVA NCHINI

SERIKALI INATHAMINI NA KUTAMBUA MCHANGO WA MADEREVA NCHINI

Arusha

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali inatambua, inaheshimu na kuthamini mchango wa madereva nchini.

Hayo ameyasema leo Agosti, 20 Waziri Mkuu wakati akifungua kongamano la tatu la madereva wa Serikali katika ukumbi wa AICC jijini Arusha amesema Serikali itaendelea kuzipatia ufumbuzi changamoto za madereva ili kuikuza kada hiyo muhimu kwa maendeleo ya nchi.

“Wizara ya ujenzi hakikisheni mnawasimamia vizuri madereva kwa kuratibu shughuli zao ili washiriki kwa wingi na kupata fursa za kujifunza masuala ya kazi zao kila mara,” amesisitiza.

Amewataka viongozi kuthamini kada ya madereva kwa kuwapa mahitaji yao ili wafanye kazi kwa ufanisi na hivyo kulinda usalama wa viongozi, wananchi na magari wanayoyaendesha.

“Zingatieni nidhamu na maadili ya udereva na utumishi wa umma kwa kujiepusha na rushwa, ulevi na uvunjifu wa sheria za usalama barabarani,” amesisitiza Majaliwa.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Majaliwa ameupongeza Wakala wa Ufundi na Umeme(TEMESA), kwa kuwa na mitambo ya kisasa ya kutengeneza magari na kuwataka kuongeza ubunifu na uadilifu ili kuleta tija katika utengenezaji wa magari ya Serikali.

Naye Naibu waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya amemhakikishia Waziri Mkuu kuwa Wizara itaendelea kusimamia na kukilea chama cha madereva ili kikue na kufanya kazi kwa weledi.

” Wizara itahakikisha madereva wanapata elimu stahiki ya magari wanayoyaendesha ili kuendenda na ukuaji wa teknolojia na kuwawezesha kushiriki vikao vyao ili kukuza weledi.

Zaidi ya madereva 1300 kutoka Tanzania bara na Zanzibar wanashiriki kongamano hilo linaloongozwa na kauli mbiu isemayo ” Dereva wa Serikali jitambue, timiza wajibu wako, usalama barabarani unaanza na wewe kazi iendelee”.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here