Home KITAIFA MAKAMBA AANIKA FURSA ZA USHIRIKIANO TANZANIA NA HANGARY 

MAKAMBA AANIKA FURSA ZA USHIRIKIANO TANZANIA NA HANGARY 

Na Esther Mnyika  

SERIKALI ya Tanzania  na Hangary wamesaini mkataba wa ushirikiano katika sekta ya maji kwa sababu nchi hiyo wanaongoza duniani kwa kudhibiti mafuriko maji taka na maji salama hivyo kupata ujuzi wa teknolojia. 

Pia nchi hiyo wanatarajia kufanya uwekezaji wa Kiwanda cha kutengeneza ndege ndogo Mkoani Morogoro. 

Akizungumza leo Machi 28 2024 jijini Dar es Salaam baada ya kusaini mkataba huo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  January Makamba amesema  ugeni huo umekuja baada  ya Rais wa Hangary kufanya ziara nchini mwaka jana.

“Tumefanya mazungumzo ya kiserikali ikiwemo ushirikiano wa kibiashara kufanya makongamano ya kibiashara nchi hizi mbili kufanya ziara za kibiashara kwa sekta binafsi.

” Pia mazungumzo mengine ni kuhusu sekta ya utalii ambapo miaka miwili iliyopita watalii walikuwa 5000 hadi sasa watalii wamefika 11000 ni ongezeko la watalii, “amesema Makamba.

Amesema wanatajia kusaini mkataba wa usafiri wa anga kuwezesha ndege kusafiri moja kwa moja  kutoka Hangary hadi Tanzania. 

Makamba amesema amesha waahidi kuwapa rasimu ya mkataba huo ili waanze safari hizo mara moja.

Vilevile,  wamezungumza namna ya kushirikiana katika elimu watanzania walio nufaika na ufadhili wa masomo 146 amba Nchi ya Hangary ilitoa ufadhili wa masomo 30 na Tanzania tano.

Ameongeza  kuwa wanatarajia kufungua uwakilishi nchini ili kuimarisha ushirikiano wa nchi hizo mbili.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Hangary, Peter Szijjàrtò amesema  walikuwa  na mazungumzo  mazuri na nchi hizo mbili zina ushirikiano katika mambo mbalimbali. 

“Tulikuwa na mazungumzo  tumezungumzia sketa ya maji, elimu, utalii na kuhusu usafiri  wa anga tutasaidia nchi ya Tanzania  katika sekta  hizo na kubadilishana ujuzi na uzoefu  kati ya Hangary  na Tanzania,”amesema Szijjàrtò.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here