Home KITAIFA DARAJA LA SIMIYU NA SUKUMA KUKAMILIKA MWAKANI

DARAJA LA SIMIYU NA SUKUMA KUKAMILIKA MWAKANI

Mwanza

NAIBU Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya amemtaka Mkandarasi China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) anaejenga daraja la Simiyu lenye urefu wa mita 150 na Barabara unganishi KM 3 na Mkandarasi Mumangi Construction Co. Ltd anayejenga daraja la Sukuma kuongeza kasi ya ujenzi wa madaraja hayo ili yakamilike mapema mwakani.

Ameongea hayo leo Agosti, 17 2024 wakati akikagua ujenzi wa madaraja hayo Mkoani Mwanza Wilayani Magu na kusisitiza umuhimu wa madaraja hayo kwa uchumi wa mikoa ya kanda ya ziwa.

“Hakuna sababu ya kuchelewesha ujenzi wa miradi hii kwani wakandarasi wote wanauwezo mkubwa hivyo TANROADS wasimamieni kikamilifu ili tupate thamani ya fedha,”amasema Mhandisi. Kasekenya.

Naibu Waziri Kasekenya amesema madaraja hayo ya kimkakati yatafungua fursa za kiuchumi hivyo kuwataka wananchi kuongeza tija ya uzalishaji ili kukuza biashara na nchi jirani.

Mhandisi Kasekenya amezungumzia umuhimu wa wananchi wanaoishi jirani na miradi hiyo kuelimishwa namna ya kunufaika na fursa za ujenzi wa miradi hiyo ili kupata ajira na kuilinda ili idumu kwa muda mrefu.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Kasekenya amekagua ujenzi wa barabara ya Isandula- Hungumalwa KM 10 inayojengwa kwa lami.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here