Home KITAIFA WAKANDARASI MRADI WA TAZA (kV 400) WATAKIWA KUKAMILISHA KAZI KWA WAKATI

WAKANDARASI MRADI WA TAZA (kV 400) WATAKIWA KUKAMILISHA KAZI KWA WAKATI

Dar es Salaam

LEO Agosti 17, 2024 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dk. James Mataragio ameongoza kikao cha Tatu cha Kamati ya Uongozi ya Mradi wa usafirishaji umeme wa msongo wa kilovoti 400 wa Tanzania- Zambia (TAZA) kilichofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam.

Kikao hicho kilichojadili utekelezaji wa mradi hadi kufikia Julai, 2024, kimewataka wakandarasi wote wanaotekeleza mradi huo kukamilisha kazi mapema kwa mujibu wa mkataba.

Mradi mkubwa wa usafirishaji umeme wa TAZA unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kilovoti 400 kutoka Iringa hadi Sumbawanga na kuunganisha Tanzania na Zambia, ujenzi wa vituo vya kupoza umeme vya Iringa, Mbeya, Tunduma na Sumbawanga pamona na mfumo wa kutoa huduma ambao utawezesha kuunganisha Bara la Afrika kwa nishati ya umeme kutoka Afrika Kusini hadi Ethiopia.

Kikao hicho kimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Wizara ya Nishati na taasisi zake pamoja na Wizara ya Fedha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here