Home KITAIFA ZIARA YA UTOAJI ELIMU YA BIMA YAENDELEA WILAYA YA MAGHARIBI

ZIARA YA UTOAJI ELIMU YA BIMA YAENDELEA WILAYA YA MAGHARIBI

Zanzibar

UJUMBE kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) ukiongozwa na Naibu Kamishna wa Bima Khadija Said umeendelea na ziara yake ya kuelimisha kuhusu matumizi ya bima na Leo hii Agosti 15, 2024 umezuru ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Magharibi na kutoa elimu kwa Masheha zaidi ya 65.

Wakati wa ufunguzi wa mkutano huo Mkuu wa Wilaya ya Magharibi A , Hamida Mussa Khamis ameipongeza TIRA kwa hatua ya kukutana na viongozi hao wa wananchi na kuwapa elimu muhimu ya bima hasa bima ya afya na kuwasihi Masheha kuwa mabalozi wazuri kwenye Shehia zao.

Naye Naibu Kamishna wa Bima Khadija amesema lengo la Mamlaka ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za bima na hivyo kuwataka wananchi hao wanapopata changamoto kuwasiliana na TIRA kupitia Kanda mpya ya Unguja inayohudumia mikoa yote ya Mjini Magharibi, Mkoa wa Kaskazini Unguja na Kusini Unguja.

Kwenye ziara hiyo TIRA pia imeambatana na Meneja anayeshughulikia maswala ya sheria kutoka Mfuko wa Bima ya Afya wa Zanzibar ambae aliwaelewesha Masheha hao juu ya umuhimu wa bima ya afya na namna ambavyo wananchi wanahudumiwa kupitia bima hiyo ikiwemo kutokua na ukomo wa kuhudumia watoto au wenza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here