Home KITAIFA MKOA WA GEITA KUFUNGULIWA KWA BARABARA ZA LAMI

MKOA WA GEITA KUFUNGULIWA KWA BARABARA ZA LAMI

Geita

NAIBU Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya amhakikishia Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi kuwa Serikali imepanga kufungua mkoa wa Geita kwa barabara za lami ili kurahisisha huduma za usafiri na uchukuzi hivyo kukuza uchumi wa Mkoa huo.

Akizungumza na wananchi wa mji wa Katoro mkoani humo Mhandisi Kasekenya amesema nia ya Serikali nikuhakikisha maeneo yote yenye uzalishaji na biashara kubwa yanafikika kirahisi kwa Barabara za lami ili kuleta tija na ufanisi kwa wananchi.

” Katibu mkuu mwaka huu tumejipanga kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami barabara za Nzera-Nkome Km 20, Mtakuja-Bukoli- Bulyanhulu-Busoka-Kahama KM 122.7 na Ushirombo-Katoro 58.3″, amesema Mhandisi Kasekenya.

Naibu Waziri huyo amewataka wakazi wa Mkoa wa Geita kutumia fursa ya ujenzi wa barabara hizo kupata ajira na kukuza shughuli za biashara, uzalishaji na huduma ili kukuza uchumi binafsi na wa mkoa wa Geita kwa ujumla.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here