Home KITAIFA WAZIRI KOMBO AJITAMBULISHA KWA RAIS WA ZANZIBAR

WAZIRI KOMBO AJITAMBULISHA KWA RAIS WA ZANZIBAR

Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar bado inahitaji wawekezaji zaidi kuja kuwekeza nchini kupitia nyanja mbalimbali.

Ameeleza kuwa zipo fursa nyingi za uwekezaji Zanzibar ambazo wawekezaji wanaweza kuja kuwekeza katika nyanja mbalimbali na kuielekeza Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuweka mkazo katika eneo hilo.

Dk. Mwinyi ameyasema hayo Agosti, 2024 wakati alipokutana na Waziri na Manaibu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika walipofika Ikulu kujitambulisha baada ya kuteuliwa hivi karibuni.

Dk. Mwinyi amesema ni vema Wizara ijikite kutafuta wawekezaji wa kuja kuwekeza nchini pamoja na kunufaika kidiplomasia na mataifa mengine. Pia ameilekeza Wizara kuangalia pia masoko mengine ya kuleta wawekezaji na watalii ikiwemo kutoka nchi za Asia na Mashariki ya Mbali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here