Home KITAIFA SERIKALI YAFANYA MAZUNGUMZO NA WAWEKEZAJI KUTOKA CHINA.

SERIKALI YAFANYA MAZUNGUMZO NA WAWEKEZAJI KUTOKA CHINA.

Mwandishi wetu 

WIZARA ya Viwanda na Biashara imefanya mazungumzo na wawekezaji  kutoka  nchini  China na kuwaonyesha fursa zinazopatikana ili waweze kuwekeza nchini na nchi iweze kunufaika kwa kupata uwekezaji,  ajira na kuongeza Pato la Taifa. 

Akizungumza leo Machi 27 jijini Dar es Salaam baada ya mazungumzo hayo Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Sempeho Manongi amesema siku ya leo wamepata wageni kutoka nchini China katika  Jimbo la Changzho ambao wamekuja kwaajili  ya kuangalia maeneo ambayo wanaweza kuleta ushirikiano.

Amesema wawekezaji hao wameletwa kwa kushirikiana na kampuni  mbili ambazo ni kampuni  ya Canopus Energy  Solutions na Amec Group katika wangeni hao wameambatana na viongozi wa serikali na wawekezaji na timu ya wataalam.

“Tumewaonyesha fursa zilizopo za viwanda  na maeneo ya uwekezaji katika sekta zote muhimu  kwa nchi yetu ili waweze kuimarisha uchumi wa  nchi.Pia wamewaonyesha maeneo mengine ya viwanda ambayo ni muhimu wanaweza kuzalisha na kutengeneza Kituo  maalumu,”amesema Manongi. 

Ameeleza kuwa katika mazungumzo hayo wamekubaliana na baadhi ya maeneo hayo hivyo wakitoka hapo wanaelekea Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),kwenda kupata taarifa ya kina kwenye masuala  ya uwekezaji  ili waweze  kuingia makubaliano  kwenye  maeneo ambayo wameona ambayo yanahitajika kwaajili ya uwekezaji. 

Manongi amesema wao wameonyesha maeneo  ya sekta ya kilimo katika  kuongeza mazao ya kilimo  maeneo  ya uzalishaji wa madini ya viwanda ambayo  ni muhimu mfano chuma

Pia wamewaonyesha maeneo mengine ya viwanda ambayo ni muhimu wanaweza kuzalisha na kutengeneza Kituo  maalumu. 

Ameongeza kuwa Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) wana maeneo  makubwa ambayo wanaweza kuwekeza uwekezaji ikiwemo Kilimanjaro machine tools, Tange lipo Tanga, Kibaha maeneo kwaajili ya uwekezaji.

Amesema wameshauriana kuna uwekezaji  wa moja kwa moja,  wa ubia na kubadilisha ujuzi na uzoefu ambao utaletwa nchini.

Aidha amesema  katika Miradi saba ikitekelezwa kuzalisha MEGAWATI zaidi ya 1400  wanahitaji umeme kwa wingi hivyo wakipata uwekezaji kikubwa kupata utalaamu wa hiyo sekta ndio wanahitaji kwa wingi na baadae wawekezaji wakijitokeza watapata umeme kwa wingi na uzalishaji utaongezeka ajira na matumizi ya umeme.

Naye Kiongozi wa Ujumbe Kutoka Serikalini  ya Jimbo la Changzho, Shen Don amesema nchi hizo mbili zimekuwa na ushirikiano  mkubwa  katika  nyanja mbalimbali  wanahitaji kuwekeza katika uzalishaji katika  viwanda. 

Kwa upande wake  Mhandisi Anna Nyangasi wa Kampuni  ya Canopus Energy  Solutions amesema  kampuni yao inajihusisha na uuzaji wa dhana za kilimo,  usafirishaji  na uzaji usambazaji bidhaa za solar.

Kupitia Kampuni mbili hizo wameaandaa uwekezaji  maeneo yafuatayo pamoja  na kilimo, afya,  vifaa vya ujenzi, vifaa vya uchakataji

“Watawekeza katika  maeneo  mashine za kilimo watawekeza dola za kimarekani milioni  24.5,  vifaa vya hospitali watawekeza dola za kimarekani milioni 6.

“Vifaa vya  umeme watawekeza dola za Kimarekani  milioni mbili vifaa vya ujenzi dola za kimarekani milioni 11.3 vifaa vya uchakataji wa mafuta dola za kimarekani milioni  43,”amesema Mhandisi Anna .

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here