Esther Mnyika, Dodoma
MBUNGE wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Sophia Mwakagenda amesema Shirika la Mawasiliano Tanzania ( TTCL) limefanya maboresho makubwa kuendana na wakati uliopo sasa kwani wanawafikishia huduma wananchi mpaka kwenye makazi yao kwa kupitia huduma yao ya fiber Mlangoni.
Hayo ameyasema leo Agosti 06,2024 Jijini Dodoma Mwakagende mara baada ya kutembelea banda la Shirika hilo lililopo kwenye maonesho ya Kimataifa ya Kilimo yanayoendelea Viwanja vya Nanenane Nzuguni.
Mwakagende amelipongeza shirika hilo kwa maboresho makubwa waliyoyafanya katika kuhudumia umma hasa katika ulimwengu wa kidigital.
“Niapongeze Serikali chini ya usimamizi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kupitia shirika hili la TCCL Kwa uwekezaji mkubwa uliofanyika tumeona sasa mtandao wa interneti unapatikana kila sehemu na ukizingatia sasa hivi Dunia ipo kiganjani,”mesema.
Amesema maboresho yaliyoafanyika wao kama jicho la pili la serikali wameridhishwa na kuahidi kushirikiana na serikali kuhakikisha mtandao wa TTCL unafika mbali zaidi.
Ameongeza kuwa ufanyaji wa biashara kwa sasa unategemea zaidi mtandao lakini pia kuanza kwa treni ya umeme SGR kunategemea zaidi mtandao haswa katika ukataji wa treni ili kupunguza msululu kwenye madirisha ya kukatia tiketi.
“Niwaombe TTCL kupeleka huduma hii kwa shule za sekondari zilizopo vijijini wapate huduma hii kwenye maktaba zao na maabara zao ili waweze kujifunza kwa vitendo”meongeza.
Mwakagenda ametoa rai kwa shirika hilo kuhakikisha wanafukisha huduma ya intaneti kwa shule za sekondari zilizopo vjijini ili kuwasaidia kujifunza.