Home KITAIFA NIC YAWEKA MIKAKATI YA BIMA YA KILIMO.

NIC YAWEKA MIKAKATI YA BIMA YA KILIMO.

Na Esther Mnyika, Dodoma

SHIRIKA la Bima Nchini ( NIC) limesema Bima ya Kilimo ndio mkombozi kwa wakulima wakati majanga ya kuharibiwa mazao.

Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa Shirika la Bima Nchini (NIC), Karimu Meshack.

Akizungumza leo Agost, 3 2024 na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa NIC, Karimu Meshack kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane yanayofanyika katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.

Amesema kuwa Kilimo kuwa na tija ni pamoja na kuwa na Bima Kilimo itayofanya wakati wa majanga kufidiwa kwa nguvu iliyotumika katika kulima mazao mbalimbali.

“Hatutaweza kuacha Kilimo kisiwe na Bima tutaonekana tupo kwa ajili kuua Kilimo hivyo NIC itakwenda bega kwa bega na Wakulima,”amesema.

Amesema Serikali ya awamu ya Sita ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan imewekeza katika kilimo hivyo NIC imekuja na Bima ya Kilimo ya kufanya Kilimo kisichokuwa na mawazo ya kufikiria majanga.

Amesema NIC imetoa bima ya kilimo Kwa asilimia 90 ya mazao yanayolimwa nchini na huduma za Bima zinapatikana katika Mikoa yote nchini.

Meshack amesema kuwa wanazo Bima zingine ikiwemo ya Maisha ya kusaidia pale unapopata majanga hata kifo.

Amesema mwanaume ambaye ana Bima ya Maisha akifariki mjane anaacha kuanguaka badala yake atalia na kitambaa laini ambapo kile kilichowekwa kinakwenda kusaidia kwendesha maisha kwa waliobaki.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here