Home KITAIFA TTCL IMEWAPELEKEA HUDUMA YA MAWASILIANO IMARA AMBAYO ITAWARAHISHIA WAKULIMA KUWASILIANA

TTCL IMEWAPELEKEA HUDUMA YA MAWASILIANO IMARA AMBAYO ITAWARAHISHIA WAKULIMA KUWASILIANA

Na Esther Mnyika, Dodoma 

AFISA Uhusiano wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Ester Mbanguka amesema wamewapelekea huduma ya mawasalino imara ambayo itawarahisishia wakulima kuwasiliana na kufuatilia masoko duniani kupitia huduma ya intaneti.

Afisa Uhusiano wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Ester Mbanguka

Akizungumza leo Agost, 3,2024 na Waandishi wa Habari Ester kwenye maonesho ya Kimataifa ya  Kilimo Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma amewaomba  wakulima kutumia huduma ya mtandao ili kuboresha kilimo lakini pia kuendana na teknolojia.

Amesema Nanenane ya mwaka  huu wameenda na huduma mbalimbali ambazo zitawasaidia wakulima hasa wanaolima kisasa kwa kutumia teknolojia.

“Tumewaletea mifumo ya teknolojia wakulima na ambao sio wakulima kwani sasa hivi Dunia yote ipo kidigitali sasa watakapofanya kilimo ni lazima wauze au watafute pembejeo za kilimo sasa wanapokuwa na huduma ya mtandao wanaweza kuwafika wauzaji na pembejeo lakini pia wanunuzi wa mazoa yao kwa njia rahisi,”amesema Ester.

Ameongeza kuwa katika maonesho hayo wamepata wateja wa huduma ya internet ambao ni waoneshaji lakini pia wamefunga interneti ya bure kwenye banda lao.

Amesema mtu anaweza kuipata bure pia kuna baadhi ya maeneo kwenye maonesho hayo wamefunga huduma hiyo bure kwa ajili ya wananchi wanaoenda kutembelea maonesho hayo.

Amesema wateja wote waTTCL nchini kutoa taarifa kituo cha huduma kwa wateja pindi wanapopata changamoto yeyote pindi wanapotumia huduma yao ili ziweze kutatuliwa kwa wakati na sio kulalamika sehemu tofauti.

“Nitoe rai kwa wateja wetu wote nchini kuripoti kituo cha huduma kwa wateja pindi wanapopata changamoto katika huduma zetu ili tuweze kuwasaidia kwa haraka lakini wanapokuwa wanazungumza pembeni wanakuwa wanabaki na tatizo na sio kutatua tatizo,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here