Home KITAIFA DIRA YA MAENDELEO YA 2050 IBEBWE NA VIJANA ZAIDI: SPIKA DK. TULIA

DIRA YA MAENDELEO YA 2050 IBEBWE NA VIJANA ZAIDI: SPIKA DK. TULIA

Mbeya

SPIKA Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Tulia Ackson ambaye pia ni Rais wa umoja wa Mabunge duniani, amewataka vijana kuchangamkia fursa ya kutoa maoni kuhusu Tanzania waitakayo ili kuweza kuwa na muafaka wa pamoja kama vijana kwa miaka 25 ijayo.

Hayo ameyasema leo Agosti, 03 Jijini Mbeya Dk. Tulia kwenye Kongamano la Kikanda, Kanda ya Kusini liliofanyika katika Ukumbi wa Eden highland J ikiwa ni muendelezo wa Wizara ya Nchi ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji kukusanya maoni ya wananchi ikiwa ni maandalizi ya uandishi wa Dira mpya ya maendeleo ya mwaka 2050.

Dk. Tulia ametoa wito huo akirejea takwimu za sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 iliyoonesha kuwa zaidi ya asilimia 77 ya watanzania wote ni watoto na vijana na hivyo kusema kuwa hatma ya Tanzania ipo mikononi mwa vijana hasa wa miaka 15-35 ambao ni asilimia 34.5 ya Watanzania wote.

“Lazima vijana muone dira hii ya Taifa ya Maendeleo ni ya kwenu na ni nafasi yenu ya kutoa maoni, kushauri na kuchangia ufanisi wa dira ya mwaka 2050.Hii dira ni ya vijana,” amesema Dk. Tulia.

Katika hatua nyingine Dk. Tulia Ackson amekiri pia umuhimu wa Wazee kutoa maoni yao katika dira hiyo kutokana na uzoefu na kufahamu mambo mengi, ambayo yalifanyika kimakosa na yale ambayo hayakufanyika kiufanisi ili kusahihisha na kuyaweka mambo hayo katika namna nzuri ili yaweze kufanyiwa kazi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here