Home KITAIFA DK. NCHIMBI AWATAKA VIONGOZI UWT KUVUNJA MAKUNDI KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA...

DK. NCHIMBI AWATAKA VIONGOZI UWT KUVUNJA MAKUNDI KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA NA UCHAGUZI MKUU 2025.

Na Mwandishi wetu

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi amewataka viongozi wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ngazi ya Mikoa,Wilaya,Kata,Matawi na Mashina kuvunja makundi,ili kuimarisha Jumuiya na Chama.

Balozi Dk. Nchimbi ameeleza kuwa Umoja na mshikamano wa viongozi wa Jumuiya ya UWT utachangia ushindi wa kishindo katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Amesema hayo wakati wa ufunguzi wa Semina ya Wajumbe wa Baraza Kuu la UWT yaliyofanyika katika Ukumbi wa NEC leo Agosti, 2 2024.

“UWT ni miongoni mwa Jumuiya zinazotegemewa kukipa Chama chetu ushindi wa kishindo,hivyo tunapoelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa mwezi Novemba mwaka huu ninawataka muvunje makundi ili kuwa na mshikamano wa kuipeperusha vyema bendera ya Chama chetu,”amesema.

Balozi Dk. Nchimbi amewataka viongozi wa UWT kuendelea kufanya ziara katika maeneo mbalimbali ngazi ya vijiji mpaka Mkoa ili kukutana na wananchi na kuwaelezea Kazi nzuri inauofanywa na Serikali ya CCM inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here