Home KITAIFA TRA IMEWAOMBA WADAU NA WANANCHI KUJITOKEZA KWA WINGI NANENANE

TRA IMEWAOMBA WADAU NA WANANCHI KUJITOKEZA KWA WINGI NANENANE

Esther Mnyika, Dodoma

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa rai kwa wakulima na wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye banda lao ili kupata elimu ya kodi lakini pia kufahamu bidhaa za kilimo zilizo kwenye msamaha wa kodi.

Wito huo umetolewa leo Agost 2,2024 jijini Dodoma na Afisa Msimamizi wa Kodi TRA, Philip Eliamini kwenye Maonesho ya Wakulima yanaendelea viwanja vya nanenane vilivyopo Nzuguni.

Amesema wamejikita kutoa elimu ya kodi kwenye maonesho hayo kwani wakulima ni wadau wazuri wa kodi na serikali imewekeza kwa kiasi kikubwa ili kumuwezesha mkulima kulima kibiashara na kuweza kulipa kodi.

“Nawasihi wakulima wafike kwenye viwanja hivi ili waweze kujifunza na kupata elimu ya msamaha kodi kwa dhana za kilimo zilizopo kwenye msamaha huo”,Amesema.

Eliamin amesema pia wanatoa huduma ya namba ya mlipa kodi (TIN NAMBA) kwa watu ambao awana lakini wanatoa huduma ya ukadiliaji kodi kwa wafanyabiashara.

Pia amesema kila mfanyabiashara mwenye mauzo ya milioni 11 kwa mwaka anapaswa kutumia mashine ya EFD.

Ameongeza kuwa maagizo yaliyotolewa na katibu mkuu wizara Uvuvi na Mifugo Profesa Shemdoe watayafanyia kazi na amewataka wadau pia kuyafanyia kazi.

Pia amewataka wadau wanaoagiza bidhaa zilizo kwenye msamaha kodi kuwasilisha nyaraka zao kwa TRA mapema kabla ya bidhaa hizo kufika lakini pia amewataka watendaji wa TRA kufanyakazi kwa bidii na weledi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here