Home KITAIFA MAVUNDE AWAONGOZA WATUMISHI MADINI, WAOMBOLEZAJI KUMUAGA NYANGE

MAVUNDE AWAONGOZA WATUMISHI MADINI, WAOMBOLEZAJI KUMUAGA NYANGE

Dodoma

WAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde amewaongoza Watumishi Wizara ya Madini na baadhi ya taasisi zake kumuaga Mtumishi wa Wizara ya Madini Afisa Hesabu Mwandamizi Humphrey Nyange aliyefariki Dunia Julai 28, 2024 katika Hospitali ya Benjamini Mkapa Jijini Dodoma alikokuwa akitibiwa.

Akizungumza leo Agosti Mosi 2024, Nyumbani kwa marehemu Meliwa jijini Dodoma, Waziri Mavunde ametoa pole kwa familia, ndugu, jamaa watumishi na marafiki na kumwelezea marehemu Humphrey kuwa mtu ambaye katika majukumu yake alihakikisha kila aliyestahili kupata haki yake anaipata kwa wakati.

Pia, amemwelezea kuwa ni mtumishi aliyejali wenzake na kutamani kutengeneza furaha kwa wenzake na kusema, “Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa zawadi ya maisha yake, alikuwa ni mtu mwenye upendo, ushirikiano na zawadi kwa wenzake,” amesema Mavunde.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here