Home KITAIFA NAIBU SPIKA ZUNGU ANATARAJIA KUWA MGENI RASMI MAHAFALI YA 19 YA CHUO...

NAIBU SPIKA ZUNGU ANATARAJIA KUWA MGENI RASMI MAHAFALI YA 19 YA CHUO CHA FURAHIKA.

Dar es Salaam

NAIBU Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Zungu anatarajiwa kuwa mgeno ya rasmi katia mahafali ya 19 ya Chuo Cha Ufundi Stadi (Furahika) ambacho kipo Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza leo Julai 29, 2024 jijini Dar es Salaam Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Dk. David Msuya  leo, amesema  mahafali hiyo inatarajia kufanyika Agosti,3 2024  jumla ya wahitimu 120 wa kozi mbalimbali.

Amesema wahitimu hao ni kozi mbalimbali ikiwemo ualimu, sekretari, hoteli na nyinginezo ambazo zipo  chini ya VETA na wahitimu waliofanya vizuri kwa kila kozi watapewa zawadi.

“Tunayofuraha kubwa  kwenda kusheherekea mahafari ya 19 tangu chuo hiki kianzishwe na mgeni wetu ataakuwa Mbunge wa Ilala, ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mussa Zungu, hivyo tunawaomba wazazi ama walezi wa vijana ambao wanahitimu mafunzo haya waje kwa wingi kufurahia kwa pamoja na watoto kwa siku hii muhimu kwa maisha yao.

“Pia mahafali haya yanafungua milango kwa kundi lingine kujiunga na muhula mpya wa masomo kwa miezi sita na mwaka mmoja kwa kozi ya hoteli, Bandari na nyinginezo na tunawaomba vijana ambao wameishia darasa la saba, kidato cha pili ama kidato cha nne na wakashindwa kupata alama nzuri za kuendelea na masomo waje hapa kutimiza ndoto zao katika elimu,” amesema.

Aliongeza kuwa muhula mpya utaanza Septemba 10 mwaka huu pamoja na kozi mpya ya Uhariri na upigaji picha za video (Video Production) itaanza kufundishwa chuoni hapo jambo linalotanua wigo wa vijana wengi kutimiza ndoto zao kwa kupata ujuzi wa kozi mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho.

Amesisitiza kuwa yote yanafanyika kutokana na Rais Samia Suluhu Hassan kufungua milango ya uwekezaji na kusababisha mashirika mengi kuja kusaidia vijana na wao kutoa elimu bure na jambo linalitakiwa sasa ni vijana kutumia fursa hiyo vizuri ili kujikomboa katika dimbwi la umasikini.

Dk. Msuya ameongeza kuwa wanafunzi ambao wanajiunga na chuo hicho wanapata fursa ya kutafutiwa sehemu ya mafunzo kwa vitendo na wale wanaofanya vizuri wanajiweka katika mazingira mazuri ya kupata ajira baada ya kumalizi masomo yao.

Aidha amewaomba wazazi na walezi wa vijana hao wanahitimu na wengineo kujitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hilo muhimu katika maisha ya watoto wao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here