Home KITAIFA DK.TULIA AMUAPISHA KOMBO LEO

DK.TULIA AMUAPISHA KOMBO LEO

Dar es Salaam

SPIKA wa Bunge Dk. Tulia Ackson leo Julai, 25 2024 amemuapisha Balozi Mohamed Thabit Kombo huku akimtaka kwenda kufanyakazi aliyokusudiwa kuifanya ili kukamilisha mipango mingi ya maendeleo iliyoanzishwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza mara baada ya kumuapisha katika Ofisi Ndogo za Bunge jijini Dar es salaam Dk. Tulia amesema kuteuliwa kwa Balozi Kombo kuwa mbunge na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ili kutumikia wananchi lakini pia kuendeleza mipango mingi ya maendeleo iliyowekwa na Rais.

“Rais Dk. Samia anamipango mingi na mingi ameiweka wazi hivyo anawategemea ninyi ili kuweza kuitekeleza kwa ustawi wa Taifa”,amesema Dk.Tulia.

Amesema uapisho aliofunya ni kwa mujibu wa kanuni ya 30(2)(b) ya kanuni za kudumu za bunge toleo la februari 2023 ambapo inatamka kuwa mbunge kabla ya kuanza kazi ataapishwa na spika.

Amesema pia sheria hiyo imempa mamlaka spika kuchangua eneo la kumuapishia kama hakuna mkutano wa bunge unaoendelea na baadae spika kutoa taarifa bungeni kwenye kikao cha kwanza.

Kombo aliteuliwa na Rais Dk. Samia kuwa mbunge na waziri Julai 21,2024 mara baada ya kutenguliwa aliyekuwa waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashiriki Januari Makamba.

Baadhi ya wabunge walioshiriki katika hafla hiyo ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dk.Stegomena Tax , Londo ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here