Home KITAIFA ISHI NYUMBA KULINGANA NA KIPATO CHAKO

ISHI NYUMBA KULINGANA NA KIPATO CHAKO

Dar es salaam

WAZIRI wa Ujenzi Innocent Bashungwa amitaka Wakala wa Ujenzi (TBA ) kuwachukulia hatua za kisheria wapangaji ambao hawalipi kodi ya jengo bila kuangalia hadhi zao kisha wapangishwe wenye uwezo wa kulipa ili kupata fedha za kutekeleza jengo la tatu na la nne (Block C na D) eneo la Magomeni Kota iliyofikia asilimia 15 ujenzi.

Agizo hilo amelitoa leo Julai 23, 2024 Jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya Ufunguzi wa nyumba za watumishi wa umma zilizojengwa na TBA eneo la Magomeni kota awamu ya pili “B” amesema baadhi ya watu wamekuwa wakipanga nyumba hizo na kukaa muda mrefu bila kulipa hivyo wanavyotolewa kwa notes hawalipi madeni yao hivyo kupelekea upotevu wa mapato ambayo yangesaidia nyumba nyingine kuendelea kujengwa.

Amesema jengo moja la ghorofa saba kwa ajili ya makazi ya watumishi wa umma katika eneo la Magomeni Kota (Awamu ya Pili ‘B’), Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Dar es salaam lililogharimu shilingi bilioni 5.687.

“TBA imekuwa ikiendelea kujenga makazi watu ili kupunguza uhitaji hivyo niwatake watu wote mtambue kama upange nyumba kulingana na uwezo wako acheni kutaka kuishi maisha ya kufahari wakati kipato ni kidogo manapanga nyumba alafu kulipa mnakuwa wasumbufu,” amesema Waziri Bashungwa.

Amesema kwa mujibu wa takwimu za TBA kuna upungufu wa mahitaji ya nyumba bora yanayofikia milioni 3 kuongezeka kwa wastani wa nyumba 390,000 kila mwaka.

Amesema wapo watumishi ambao wanasubiri majengo hayo yakamilike ili waweze kupanga.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Mkuu TBA, Arch Daud Kondoro amesema Serikali ilitoa kiasi cha bilion 5.687 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa jengo la makazi kwa ajili ya watumishi wa Umma eneo la Magomeni Kota awamu ya pili hadi kukamilika kwake .

Ameongeza kuwa kazi zote katika mradi huo zikijumuisha ubunifu, ujenzi na usimamizi zimetekelezwa na Wakala wa Majengo Tanzania kwa kutumia Wataalam wake wenyewe.

“Kwa ujumla ubunifu na usanifu wa mradi huu ulizingatia mabadiliko chanya ya ukuaji katika Sekta ya Uchumi, Mipango Miji na Teknolojia ya Ujenzi, Mawasiliano na Miundombinu uliopatikana hapa nchini,”amesema.

Amesema ujenzi wa jengo hilo ulianza Novemba mwaka 2022 umezingatia Kanuni na viwango bora vya majengo ya serikali.

Amesema eneo hilo la Magomeni Kota lina viwanja vitatu vyenye ukubwa wa jumla ya Hekta 12.95 (sawa na ekari 32 au mita za mraba 129,499.41).

Pia amrongeza kuwa ujenzi huo ulianza rasmi Novemba 2022 na ni utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi CCM ya mwaka 2020 hadi 2025 ibara ya 55(h) inayoelekeza maeneo yaloyorejeshwa serikalini na kuwa chini ya TBA kutoka ofisi ya Rais Tamisemi kuendelezwa kwa utaratibu hivyo wanakwenda kujenga nyumba za kisasa Kawe,Masaki, Dodoma ili kukidhi mahitaji uhaba wa makazi .

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila amewashauri wananchi wake kuishi kulingana na hali ya vipatao vyao kwani baadhi ya wakazi waliowekwa katika nyumba za Kota wale 644 miongoni mwao wameleta malalamiko ya kishindwa kumudu baadhi ya gharama ikiwemo maji, umeme, usafi hivyo anashindwa hata namna ya kuwasaidia kwakuwa walipewa ofa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here