Home KITAIFA UWT YAKERWA NA KASI NDOGO YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA CHUO CHA...

UWT YAKERWA NA KASI NDOGO YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA CHUO CHA UFUNDI STADI (VETA) KAKONKO

Kigoma

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa Mary Chatanda (MCC) amekasirishwa na kusuasua kwa utekelezaji wa mradi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Kakonko.

Serikali ya CCM ilibuni na kuanza kutekeleza ujenzi wa chuo hiki kwa lengo la kuongeza na kupanua wigo wa ajira kwa vijana, ambapo jumla ya shilingi bilioni 1.4 za kitanzania zilitengwa ili kukamilisha mradi huu ifikapo tarehe 21 Disemba 2023. Lakini, mradi huu bado haujakamilika mpaka hivi sasa.

Chatanda amewataka viongozi wote wanaosimamia mradi huu kuhakikisha wanaukamilisha bila kuleta visingizio.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here