Home KITAIFA BASHE: AFANYA UKUGUZI MAGHALA SUMBAWANGA

BASHE: AFANYA UKUGUZI MAGHALA SUMBAWANGA

Rukwa

WAZIRI wa Kilimo, Hussein Bashe amefanya ziara ya ukaguzi katika maghala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) yaliyopo eneo la Mazwi, Sumbawanga mjini, mkoani Rukwa Julai 16 2024.

Katika ziara hiyo, Meneja wa Kanda ya Sumbawanga NFRA, Marwa Range ameeleza kuwa uwezo wa kuhifadhi nafaka za mahindi katika eneo la Mazwi ni tani 28,500 ambapo zoezi la ununuzi linaendelea katika maghala hayo.

Waziri Bashe alipata wasaha wa kukagua mizani ya digitali ambayo imeanza kutumika na kujiridhisha na shughuli ya upimaji wa nafaka unaondelea.

Aidha, ameelekeza mizani iongezwe ili kuharakisha zoezi la upimaji kama sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan mapema leo wakati wa uzinduzi wa maghala ya NFRA katika eneo la Kanondo.

Waziri Bashe amefurahishwa kuona Wakulima mbalimbali wakiwasilisha mazao yao kwa maghala ya Mazwi na kusisitiza kasi ya upimaji iongezwe.

Vile vile, amemuelekeza Mtendaji Mkuu wa NFRA Dk. Andrew Komba, Afisa kukarabati maghala hayo ili huduma kwa Wakulima zisikwame.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here