Home KITAIFA CBE KUTOA MASTERS KWA NJIA YA MTANDAO

CBE KUTOA MASTERS KWA NJIA YA MTANDAO

Dar es Salaam

MKUU wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Profesa Tandi Luoga amesema chuo hicho kwa sasa kimekuja kivingine kwani kimeanza kutoa masters kwa njia mtandao.

Pia kimewakaribisha wananchi wote wenye sifa na vigezo kuomba nafasi za masomo katika chuo hicho.

Akizungumza Julai ,11 2024 na waandishi wa habari Profes Luoga wakati alipotembelea banda hilo kwenye Maonesho ya 48 ya kimataifa ya Biashara sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya mwalimu Julias Nyerere Jijini Dar es salaam.

“Kwa sasa tuna wanafunzi wanaoshiriki masomo kwa njia ya mtandao ambapo mahali popote walipo wanapata masomo yao,”amesema

“Chuo hichi kina kozi nyingi kwa ngazi mbalimbali zikiwemo za mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi ambapo katika mafunzo ya muda mrefu wanaotoa elimu kuanzia ngazi ya cheti ,diploma,bachelor na masters,”amesema .

Amesema Kupitia programu hiyo inakwenda kumrahisishia mtumishi kusoma bila kuathiri shughuli zake programu hiyo ya mtandaoni imeanza Machi mwaka huu kutokana na mabadiliko ya teknolojia katika kurahisisha mambo.

Aidha amesema Chuo hicho chenye matawi manne katika mikoa ya Dar Es Salaam ,Dodoma,Mwanza na Mbeya kimefikia maamuzi huo wa masomo mtandaoni ili kutoa wigo mpana hasa kwa watumishi na makundi mengine kujiendeleza kielimu.

Amesema mwanafunzi wa Masters anayesoma kwa njia ya mtandao , hahitaji kwenda mpaka CBE Mwanza,Dodoma Mbeya au Dar Es Salaam kusoma isipokuwa wakati wa mitihani ambapo mwanafunzi anaenda kwenye Tawi lolote la chuo hicho lililo karibu naye.

“Hatua hii imesaidia kusambaza elimu ya biashara ndani na nje ya Tanzania, lakini imepunguza gharama kusafiri na malazi kwa mwanafunzi husika.”amesisitiza

Aidha amesema chuo hicho kimekuwa kikitoa mafunzo ya muda mfupi mfupi kwa wajasiliamari na wafanya biashara ambapo katika mafunzo hayo tunasamabaza matokeo ya tafiti ili waweze kuyaelewa na kuyatumia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here