Home KITAIFA WAZIRI KAIRUKI ASISITIZA KUONGEZA UBUNIFU NA ARI YA UTENDAJI KAZI

WAZIRI KAIRUKI ASISITIZA KUONGEZA UBUNIFU NA ARI YA UTENDAJI KAZI

Dar es Salaam

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Angelah Kairuki amewataka watendaji Makumbusho na Malikale kuongeza ubunifu kwenye maonesho mbalimbali ili kuwavutia wananchi na watalii wengi kutembelea na kujifunza kwa ufasaha Utalii wa Utamaduni unaopatikana hapa nchini.

Mhe.Kairuki amesema hayo leo Julai, 52024 wakati alipotembelea banda la Wizara ya Maliasili na Utalii kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Kairuki ameongeza kuwa ni umuhimu kutumia fursa mbalimbali zinazotokana na mwingiliano wa Taasisi za Serikali zilizopo na makampuni binafsi yanayoshiriki kwenye Maonesho hayo kwa lengo la kukuza mahusiano yatakayoleta tija.

Aidha, Waziri Kairuki amepongeza jitihada zinazofanywa na Watendaji wa Wizara hiyo katika utoaji huduma kwa wananchi katika wakati huu wa maonesho na kuwaasa kuongeza ari ya kufanya kazi kwa bidii ili Wizara hiyo iendelee kuwa kinara kwenye kuongeza pato la Taifa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here