Home KITAIFA CHATANDA ASHIRIKI MJADALA WA UANZISHWAJI WA DAWATI LA JINSIA KATIKA VYAMA VYA...

CHATANDA ASHIRIKI MJADALA WA UANZISHWAJI WA DAWATI LA JINSIA KATIKA VYAMA VYA SIASA

DAR ES SALAAM

MWENYEKITI wa Jumuiya UWT Taifa Mary Chatanda Julai,3 2024 ameshiriki Mjadala wa uanzishwaji wa dawati la jinsia ndani ya vyama vya siasa na Namna Vyama vya Siasa vinaweza Kutekeleza sera ya Dawati la jinsia ndani ya Vyama vyao.

Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Four Point – Dar es Salaam na kimeratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Kwa kushirikiana na National Democratic Institute (NDI).

kikao hicho kilichohudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa, na Taasisi za Kiraia WiLDAF, LHRC, TAMWA, TAWLA, TGNP na TWP-Ulingo kilifunguliwa na Mhe Jaji Francis S. K. Mutungi Kwa kuwaasa Wanawake kuwa linapofika suala la Mwanamke basi Wanawake wote wasimame Kwa Umoja na Kwa nguvu Moja pasipo kujali itikadi za vyama vya siasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here