Home KITAIFA VIONGOZI WA UWT TAIFA WATEMBELEA MAONESHO YA 48 YABIASHARA YA KIMATAIFA SABASAB

VIONGOZI WA UWT TAIFA WATEMBELEA MAONESHO YA 48 YABIASHARA YA KIMATAIFA SABASAB

Dar es Salaam

JUMUIYA Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) imeipongeza Serikali kwa kuandaa mazingira wezeshi na kutoa fursa kwa wafanyabiashara wazawa kukuza mitaji na kutanua soko la biashara ndani na nje ya nchi.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda (MCC) leo Julai 4,2024 alipotembelea mabanda ya wajasiriliamali kwenye maonesho ya 48 ya biashara ya kimataifa katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Wakati huohuo Mwenyekiti Chatanda aliwahimiza wajasiriamali hao kuchangamkia fursa za mikopo iliyoandaliwa na Serikali kutoka katika Halmashauri zao,mikopo itakayowasaidia kutanua na kuimarisha biashara zao

Mwenyekiti Chatanda aliongozana na Katibu Mkuu wa UWT,Suzan Kunambi (MNEC), ambapo pamoja na mabanda menginee,walitembelea banda la Mama Anna mkapa lenye wajasiriamali Wanawake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here