Na Esther Mnyika, Dar es Salaam
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imetangaza kuendelea kwa ukomo wa riba ya asilimia 6 katika robo tatu ya mwaka 2024 kati yake na benki za biashra nchini.
Pia riba hiyo itatumika kwa kipindi cha robo tatu ya tatu kuanzia Julai, 4 hadi Septemba mwaka huu.
Akisoma taarifa hiyo leo julai 4 jijini Dar es Salaam Naibu Gavana wa BoT wa (Sera za Uchumi na Fedha), Dk. Yamungu Kayandabila kwa niaba Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania BoT, Emmanuel Totuba ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Sera ya Fedha.
“Kamati ya Sera ya Fedha (MPC ) ya Bodi ya Wakurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania imeamua riba ya Benki Kuu CBR kuendelea kuwa asilimia 6 kwa robo mwaka itakayoisha Septemba mwaka huu,”amesema Dk. Kayandabila.
Amesema uamuzi huo umefanikiwa katika kikao kili chokfanyika Julai,3 2024 tathimini ya kamati kuhusu mwelekeo wa uchumi na vihatarishi mblimbali inaonesha kwamba utekelezaji wa sera ya fedha kwa kipi cha Januari hadi Juni mwaka huu wamefanikiwa kudhibiti mfumuko wa bei na kubaki chini ya lengo la asilimia 5.
Amesema maamuzi ya kamati yamezingatia mtazamo chanya wa uchumi wa dunia ambapo matarajio ni kuendelea kupungua kwa mfumuko wa bei katika nchi nyingi kuimarika kwa ukwasi katika msoko ya fedha duniani na kushuka kwa bei za bidhaa katika soko la dunia.
Amesema Kamati hiyo inatarajia uchumi wa ndani kuendelea kukua kwa kasi na upatikanji wa chakula cha kutosha na kupungua kwa kasi ya kushuka thamani ya shilingi kufuatia ongezeko la mapato ya fedha za kigeni kutokana na shughuli za utalii,pamoja na mauzo ya dhahabu na mazao ya biashara na chakula.
“Katika kuthamini mwenendo wa uchumi wa dunia kamati imebaini kuimarika kwa shughuli za kiuchumi katika nchi nyingi kwa robo ya kwanza na y pili ya mwaka 2024.
Mfumuko wa bei unaendelea kupungua na kuimrika kwa ukwasi katika masoko ya fedha duniani na Benki Kuu katika nchi nyingi kuanza kupunguza viwango vya riba ikiwemo bei ya mafuta hgafi licha ya kuongezeka kidogo mwishoni mwa mwezi Juni 2024 huku bei ya dhahabu inaendelea kuwa juu ikiashiria dhahabu kuendelea kutumika kama uwekezaji mbadala katika mazingira y kushuka kwa thamani ya sarafu mbalimbali kutokan na migogoro ya kisiasa duniani,”ameeleza.
Amesema kuwa matarajio ni uchumi wa dunia kuendelea kuimarika kipindi kilichobaki cha mwaka 2024 na 2025 pamoja na kuwepo kwa hatari ya kuongezeka kwa migogoro ya kisia na mizozo ya kibiashara.
Dk. Kayandabala amesema kuhusu mwenendo wa uchumi nchini kamati imeridhishwa na kuendelea na kuimarika kwa shuguli za kiuchumi kutokana na utekelezaji wa sera thabiti na maboresho mbalimbali yenye lengo la kukuza uchumi.
Akizungumzia kuhusu kushuka thamani sarafu tamesema kwa Tanzania imeshuka kwa kiasi kidogo sawa na asilimia 11 ikiwa tofauti na nchini zingine ni asilimi 30 na mfumuko wa bei asilimia 20 asilimia 30 hadi asilimia 50 hivyo Tanzania na Uganda mfumoko wa bei ni mdogo chini ya asilimia 5.