Home KITAIFA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII,JINSIA,WAZEE NA WATOTO ZANZIBAR YAFANYA ZIARA KIVULINI

WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII,JINSIA,WAZEE NA WATOTO ZANZIBAR YAFANYA ZIARA KIVULINI

Mwanza

KATIBU Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto Zanzibar, Abeida Rashidi Abdallah amesema wanaamini ziara yao ya mafunzo katika shirika la kivulini lililoko Jijini Mwanza, itakuwa na tija kubwa maaana watapata mbinu za ainatofauti kutoka kwa shirika hilo.

Akizungumza leo Julai, 3 2024 mara baada ya mafunzo ya namna ya kutokomeza ukatili kwa wanawake na watoto,nao baadhi ya washiriki wa mafunzo ya ziara hiyo wamesema shirika la kivulini wanauzoefu wa muda mrefu wa kupambana na vitendo vya ukatili.

Aidha wameongeza kuwa licha ya Serikali visiwani Zanzibar kuendeleea na kampeni mbalimbali visiwani humo lakini Serikali imeona nivema wakapata mbinu zaidi kutoka kwa shirika la kivulini ambazo zitawasaidia zaidi katika kutokomeza vitendo hivyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa shirika la kivulini Yassin Ally amesema ziara ya Katibu Mkuu na timu yake itawawezesha kujua mbinu mbali mbali za kupambana na ukatili pia wataweza kujifunza namna jamii na makundi mbalimbali wanavyoshiriki kupinga ukatili,

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Wazee atakuwa ziara ya kikazi ya siku 3 mkoani Mwanza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here