Home AFYA MUHIMBILI NA AbbVie KUBORESHA HUDUMA ZA UTOAJI GANZI NA ICU ZA WATOTO

MUHIMBILI NA AbbVie KUBORESHA HUDUMA ZA UTOAJI GANZI NA ICU ZA WATOTO

Na Beatrice Mushi-MNH

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH) imeendelea kuboresha utoaji huduma ya dawa za usingizi na ganzi pamoja na dawa za kusaidia kukomaza mapafu kwa watoto wanaozaliwa kabla ya wakati ili yaweze kufanya kazi yake kwa ufanisi.

Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Mohamed Janabi ameyasema hayo leo Jilai,2 2024 jijini Dar es Salaam alipokutana na kampuni ya AbbVie watengenezaji wa mashine za kutolea dawa ya usingizi na ganzi pamoja na dawa za kusaidia kukomaza mapafu kwa watoto wachanga ya nchini Marekani ambayo pia ina ushirika nchini Afrika ya Kusini.

Profesa Janabi ameishukuru kampuni hiyo kwa misaada mbalimbali ikiwemo mashine za kusaidia kutoa dawa za usingizi 11 zilizotolewa kwa MNH mwaka 2022 zikiwa na thamani ya shilingi milioni na kuendelea kuzifanyia matengenzo kinga kwa gharama zao wenyewe tangu kwamako huo sawa na shilingi milioni tisa kwa kila mashine kwa mwaka.

Aidha, kampuni hiyo imekua ikotoa mafunzo ndani na nje ya nchi kwa wataalam wa MNH jinsi ya kufanya matengenezo kinga ya vifaa tiba na utoaji huduma kwa watoto wachanga waliolazwa ICU ya watoto wachanga (NICU) pamoja na ICU ya watoto (PICU).


Kwa upande wake Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa kampuni hiyo Tony ameahidi kuendelea kushirikiana na MNH ili kuimrisha ubora wa huduma katika eneo la utoaji dawa za usingizi na ganzi pamoja na watoto wanaozaliwa kabla ya wakati.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here