Home BIASHARA WATANZANIA TUMIENI FURSA MAONESHO YA 48 YA SABA SABA

WATANZANIA TUMIENI FURSA MAONESHO YA 48 YA SABA SABA

Dar es Salaam

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji ametoa wito kwa Watanzania kushiriki
Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF) ya mwaka huu ili kujifunza na kubadilishana uzoefu na washiriki wa ndani na nje ya nchi.

Akizungumza Julai 2, 2024 mara baada ya kutembelea mabanda mbalimbali ya Maonesho hayo, akiwa ameambatana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Balozi John Simbachawene, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Biashara wa Wizara,Sempeho Manongi na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania, Latifa Mohamed

Aidha, Dk. Kijaji amesema Maonesho hayo yamekuwa mfano wa kuigwa kwa sababu yamekidhi viwango vya kimataifa kwa sababu waonyeshaji kutoka nje ya nchi wameongezeka tofauti na ilivyokuwa awali.

Aidha, amebainisha kuwa Maonesho hayo yanatoa fursa mbalimbali kwa Watanzania kujifunza kutoka kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ambapo nchi 26 zimeshiriki maonesho hayo ambazo zitaonyesha bidhaa zao mbalimbali.

” Nchi hii ni ya viwanda hivyo kwenye Maonesho hayo kuna viwanda vingi vimeshiriki lengo ni kubadilishana uzoefu,”amesema Dk. Kijaji

Vilevile, amebainisha kuwa Maonesho hayo yatafunguliwa Julai 3, 2024 na Marais wawili ambao ni Rais Dk. Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa J Msumbiji, Filipe Nyusi ambaye ndio Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Maonesho hayo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here