Home KITAIFA WANAFUNZI KUTEMBELEA MAKUMBUSHO YA TAIFA SABASABA

WANAFUNZI KUTEMBELEA MAKUMBUSHO YA TAIFA SABASABA

Dar es Salaam

WANAFUNZI kutoka mikoa mitano Bara na Visiwani Julai, 5 2024 wanatarajia kutembelea Makumbusho ya Taifa kwa kushirikiana Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE) ili kupata ujuzi zaidi kwa vitendo.

Hayo yamebainishwa leo Julai,1 2024 na Afisa Utamaduni wa Makumbusho ya Taifa la Tanzania, Chance Ezekiel wakati Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,anayeshughulikia Utalii, Nkoba Mabula alipotembelea banda lao lilopo kwenye maonesho ya 48 maarufu kama sabasaba.

Amesema wanafunzi kutoka Zanzibar hadisa sasa wanafunzi watakaokuja ni 22 na bara wanafunzi 12 bado wanaendelea kujisajili wataendelea kuongezeka kadili ya siku zinavyosogea.

“Wanafunzi watakiwa kujifunza vitu mbalimbali kwa vitendo kwasababu shule wanasoma kwa nadharia wanatakiwa kutembelea Makumbusho ya Taifa mbalimbali ili waone kwa uhalisia na kujifunza, “amesema Ezekiel.

Ameongeza kuwa wana Urithi usio shikika wa uchanja Chale na ndonya wa kabila la makonde umehifadhiwa kidigitali na kutoa nafasi kwa mtazamaji kupiga picha kupitia mitandao ya kijamii na kufurahia na marafik zake kwa teknolojia ya “Agumented Realty” (AR)

Ameeleza kuwa wanafungua fursa za uwekezaji na biashara kwa watanzania kwenye maeneo ya mali kale na makumbusho ikiwemo biashara ya vyakula na huduma mbalimbali kwa watalii pamoja ujasiriamali wa bidhaa za kiutamaduni na asili ya Mtanzania.

Aidha amesema utalii wa matasha ya Utamaduni kwa watalii wa ndani na nje ya nchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here