Dodoma
BARUTI haitakiwi kuhifadhiwa kwenye makazi ya watu kwasababu inaweza kuripuka kwa moto, joto, tayari moto wa gasi au umeme.
Hayo yamesemwa na Mhandisi Mgodi wa Geita Gold Mines GGM, Katambala Abeli wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika Banda la Chamber of mines huko Dodoma kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Madini mwaka 2024 katika viwanja vya ukumbi wa Jakaya Kikwete convention center.
Amesema kwasababu wapo kwenye wiki ya madini ambapo hukutanishwa na Wachimbaji wameona wazungumzie hatari iliyo katika baruti.
“Baruti ni moja ya nyenzo kuu inayotumika kuvunjia miamba migodini, katika Mgodi hauwezi kuvunja miamba mpaka utumie baruti,” amesema Katambala.
“Baruti ina madhara makubwa isipohifadhiwa katika mazingira na hali stahiki kama sheria za nchi zinavyoonyesha kwani haitakiwi kuwekwa pamoja na makazi ya watu kwani inaweza kuripuka,”amesema.
“Vitu vinavyoweza kusababisha kuripuka ni pamoja na moto, joto, mlipuko wa gasi, mtikisiko wowote na kama tunavyojua matukio mengi ya kilipuko yanayotokea duniani kwasababu ya milipuko ya baruti.
“Kama tukio la Beiruti na mengineyo yanaweza kutokea ni mlipuko mkubwa unaoweza kutokea na kusababisha madhara makubwa kwa jamii kama kupoteza maisha, kupoteza viungo na kusababisha uharibifu wa Mali na rasrimali nyinginezo,”amesema.
Amesema baruti zinatakiwa zihifadhiwe katika maeneo maalumu yanayoitwa magazini sehemu ambayo ni mbali na makazi ya watu inakuwa imetengwa kwa kuzungushia fensi au ukuta maalumu kwaajili ya kutunza baruti ili kuzuia watu kuzifikia hata kuiba hizo baruti.
Amefafanua kuwa eneo liililotengwa kwa kuhifadhia baruti linatakiwa kuwa na vifaa maalumu vya kuzuia miripuko kama radi isipige hayo maeneo na wala hayatakiwi kuwa na umeme na ndio maana kataza jamii isitunze baruti majumbani kwasababu kwenye majumba tunatumia vitu vya kupikia kama gasi, moto na umeme ambapo vyote hivyo ni hatari havitakiwi kuwa karibu na baruti.
Afisa Mahusiano wa kitengo Cha mawasiliano na uhamasishaji wa Tanzania Chamber of Mines Muki Msami amesema wanatoa elimu ya usalama kazini hasa migodini kwa kutumia Wataalamu wa aina mbalimbali walionao.
Msami amesema kazi ya Chamba ya Migodi ni kufundisha jinsi ya huifadhi wa vifaa vya milipuko kemikali na usalama migodini ili wachimbe Madini kwa usalama katika migodi yao na usalama wa jamii kwa ujumla.