Na Ashrack Miraji Same Kilimanjaro
WANANCHI wa Kata ya Kibosho,wilayani Moshi Mkoa wa Kilimanjaro,wameungana na wadau wa maendeleo kushiriki katika ujenzi wa daraja linalounganisha vijiji vitatu.
Daraja hili litawezesha wakazi zaidi ya 6,000 kupata huduma za kijamii na kuwezesha watoto kwenda shuleni.
Veridiana Mmasy, mmoja wa wadau wa maendeleo, ametoa wito kwa serikali kushirikiana na wananchi katika ujenzi wa madaraja ya kudumu.
Amesisitiza kuwa madaraja ya muda mfupi yanachoka baada ya muda, na hivyo wananchi wanahitaji vivuko vya kudumu ili kupata huduma bora.
Mwenyekiti wa vijana nguvu kazi, Alfred Shiwa, ameishukuru serikali na Mama Maendeleo kwa kushirikiana na wananchi katika ujenzi wa madaraja.
Wananchi hao waliojitolea kwa kushirikiana na Mama Maendeleo kujenga daraja litakalounganisha kijiji cha Singa na Kilima.
Pia Wamemwomba Mbunge wa Moshi Vijijini kuendelea kuwasaidia ili waweze kupata madaraja ya kudumu katika Kata ya Kibosho Mashariki.
“Tunatumai kuwa serikali itazingatia ombi la wananchi na kushirikiana nao katika kuboresha miundombinu na kuleta maendeleo katika eneo hilo. Kwa pamoja, tunaweza kujenga jamii yenye vivuko vya kudumu na huduma bora za kijamii” amesema Shiwa.