Home KITAIFA WAKULIMA WA ZAO LA PAMBA WILAYANI BARIADI MKOANI SIMIYU WAPONGEZA MRADI WA...

WAKULIMA WA ZAO LA PAMBA WILAYANI BARIADI MKOANI SIMIYU WAPONGEZA MRADI WA BBT KATIKA ZAO HILO.

NA Mwandishi wetu, Bariadi

WAKULIMA wa zao la Pamba Bariadi mkoani Simiyu wameipongeza Serikali kwa kuwaletea vijana wa Mradi wa Jenga kesho iliyo Bora ( BBT ) kwa kuwapatia elimu ya kilimo bora ya zao la pamba ambayo imewasaidia kupata mavuno mengi.

Wakulima hao wakizungumza na Lajiji Digital katika mahojiano maalum yaliyofanyika kwenye mashamba ya pamba yaliyopo katika kijiji cha Penyasosi wilayani humo wamesema, awali walikuwa wakipanda mbegu za pamba shambani ya bila kufuata mistari hali ilyopelekea kupata mavuno machache.

” Tangu wamekuja hawa vijana wa BBT na kuanza kutoa elimu ya kilimo bora cha zao la pamba tumekuwa na mabadiliko makubwa katika mashamba yetu mavuno yameongezeka sana tumelima hekali chache lakini mavuno ni mengi,” amesema George Buluba mkulima kijiji cha Penyasosi.

“Kabla ya kupewa elimu hii ya kilimo cha pamba nilikuwa na uzoefu ambao nilikuwa nao kulingana na jinsi nilivyoelekezwa na wataalam mbalimbali waliopo katika kijiji hiki,kwakweli elimu waliyonipa hawa vijana wa BBT wamenifundisha jinsi ya upandaji wa pamba kwa kufuata mistari kwa ujumla nimefundishwa utaalam mkubwa sana tofauti na awali,”Piter Mkomba – Mkulima wa kijiji cha Penyasosi.

Afisa kilimo Mradi wa BBT katika kijiji cha Nguliati Kata ya Nguliati wilayani Bariadi, Agineta Ngamba amesema,mradi huo umekuwa na manufaa makubwa katika kijiji hicho kwa wakulima kwa kuwapatia elimu mbalimbali ya kilimo cha zao la pamba na wakulima wamekuwa na mwitikio mkubwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here