π Kapinga apeleka shangwe za umeme Maswauya na Mdilu Singida Kaskazini
π Asema hayo ni matokeo ya uchapakazi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan
π Mbunge apongeza Serikali kwa miradi ya maendeleo
NAIBU waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema kuwa zaidi ya shilingi bilioni 80 zimetumika kutekeleza miradi ya usambazaji umeme vijijini mkoani Singida na hivyo kuboresha huduma za kijamii na uchumi kwa wananchi vijijini.
Kapinga amesema hayo mara baada ya kuwasha z katika Kijiji cha Maswauya na Mdilu, Wilaya ya Singida Kaskazini mkoani Singida
Akizungumza na Wananchi wa vijiji hivyo, Kapinga amesema lengo la Serikali ya Awamu ya Sita ni kuhakikisha inapeleka umeme kwenye Vijiji na Vitongoji vyote ambapo katika mwaka wa fedha 2024/2025 Serikali imetenga fedha ya kupeleka umeme kwenye vitongoji 400.
βSerikali inafahamu kuwa kuna vitongoji ambavyo havina umeme lakini maendeleo ni hatua, ilikuwa lazima umeme ufike katika vijiji vyote Tanzania na kisha usambae vitongojini, niwahakikishie kuwa Serikali itapeleka umeme kwenye maeneo yote,β amesisitiza Kapinga
Ameeleza kuwa, kazi nzuri inayofanyika ya usambazaji umeme mijini na vijijini ni matunda ya uchapakazi wa Rais, Dk. Samia Suluhu Hassan na maono yake ambayo yamewezesha umeme kusambaa kwenye maeneo hayo ikiwemo vijiji 80 vilivyosambaziwa umeme Singida Kaskazini huku vijiji Vinne tu vikisalia ambavyo ifikapo Juni 15, 2024 vitakuwa vimewashiwa umeme.
Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini,Ramadhani AlIghondo amesema kuwa, Rais Dk. Samia ametekeleza kwa ufanisi miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kufikisha huduma ya umeme katika vijiji ,miradi ya maji, miradi ya afya na elimu na kwamba wamepokea kiasi cha shilingi bilioni 4 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na Madawati.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Singida Kaskazini, Godwin Gondwe ameahidi kufuatilia utekekezaji wa miradi hiyo ya umeme vijijini ikiwemo kuhakikisha kuwa umeme unafika kwenye maeneo yanayotoa huduma kwa jamii ikiwemo zahanati.