Na Boniface Gideon -TANGA
CHUO cha Ubaharia Nchini cha Dar es Salaam Maritime Institute (DMI), kimewataka Vijana kuchangamkia fursa za masomo ya Ubaharia ili kuingia kwenye soko la ajira kwa wakati,hii inatokana na kada hiyo ya Ubaharia kuwa na fursa nyingi za ajira ndani na nje ya Nchi.
Afisa Usafirishaji Majini ambaye pia ni Mhadhiri wa DMI Kapteni Mohamed Kauli, amewaambia Waandishi wa Habari Mei 30wakati wa maadhimisho ya wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu inayofanyika mkoani Tanga katika viwanja vya Popatilal ,kuwa fursa za ajira katika Sekta za usafirishaji majini ni nyingi katika soko la ajira ndani na nje, hivyo nivyema Vijana wakachangamkia masomo ya Ubaharia,
“Chuo chetu kinatoa Elimu na Ujuzi katika Sekta za usafirishaji majini,tunawandaa wahitimu kuanzia ngazi ya chini hadi ya juu kuwa watumishi bora katika Sekta ya Majini, lakini pia tunawatafutia ajira ndani na nje ya Nchi katika Mataifa ambayo tunafanya nao kazi,”amesisitiza Kapteni Kauli
Amesema kuwa kwasasa hakuna janja janja za kuingia kwenye Sekta za Ubaharia kama zamani.
“Ni waambie tu hasa Vijana, kwasasa hakuna janja janja za kuingia kwenye Sekta za Ubaharia bila kusomea, zamani watu walikuwa wanazamia lakini kwasasa hata ukifoji cheti tu unakamatwa wakati wa uhakiki wa vyeti, hivyo niwaombe mchangamkie masomo haya,” amesema Kauli
Kwaupande wake Mwanafunzi wa chuo hicho Masaka Julius ambaye amebuni Mtambo wa Roboti kwaajili ya kubeba mizigo viwandani amesema kwakupitia mafunzo mbalimbali waliyoyapata wanauwezo wakwenda kujiajiri wenyewe,
“Kupitia mafunzo tuliyapata chuoni na kama mnavyoona hapa tumeweza kubuni mitambo mbalimbali ambayo inasaidia katika shughuli za kila siku, hususani viwandani,hivyo tukitoka chuoni tuna uhakika wa ajira hasa kwakujiari,”amesema