Home KITAIFA RAIS DK.MWINYI AWAKARIBISHA WAWEKEZAJI KUTOKA UFARANSA KUWEKEZA ZANZIBAR

RAIS DK.MWINYI AWAKARIBISHA WAWEKEZAJI KUTOKA UFARANSA KUWEKEZA ZANZIBAR

Na Mwandishi wetu, Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi ametoa wito na kuwakaribisha wafanyabiashara kutoka Ufaransa kuangalia fursa kuwekeza Zanzibar katika maeneo mbalimbali.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipofungua Mkutano wa majadiliano ya fursa za uwekezaji kati ya Ufaransa na Zanzibar kutoka kwa ujumbe wa Wafanyabiashara wa makampuni 20 ya Ufaransa katika ukumbi wa Hoteli ya Park Hyatty Zanzibar Mei, 29 2024.

Aidha amesema sera kuu ya uchumi wa Zanzibar ni uchumi wa buluu hivyo amewakaribisha kuangalia fursa za kuwekeza katika sekta ya utalii wa fukwe, urithi, michezo na mikutano, sekta ya bandari, mafuta na gesi, sekta ya bandari ikiwemo ya makontena , uvuvi pamoja na meli za usafirishaji wa mizigo na abiria.

Pia amebainisha fursa za miradi ya miundombinu ikiwemo barabara, viwanja vya ndege , sekta ya nishati na maji, pamoja na kilimo cha viungo.

Rais Dk.Mwinyi amewahikikishia wawekezaji hao kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeweka mazingira mazuri kikamilifu ya kufanya biashara na uwekezaji.

Ujumbe huo pia uliambatana na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui , Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Ali Mwadini na Mwenyekiti wa Shirika la Kimataifa la MEDEF kutoka Ufaransa, Gerald Wolf.

Viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo Mawaziri na sekta binafsi wameshiriki mkutano huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here