Home KITAIFA MKATABA WA TANESCO NA SONGAS KUMALIZIKA JULAI 2024.

MKATABA WA TANESCO NA SONGAS KUMALIZIKA JULAI 2024.

Na Mwandishi wetu Dodoma

SERIKALI imesema kuwa mkataba wa ununuzi wa umeme kati ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na SONGAS utafikia ukomo Julai 31 mwaka huu, na kwamba wameunda timu ya wataalam (Government Negociation Team – GNT) iliyoanza majadiliano mwezi Aprili, 2023 na inatarajia kukamilisha majadiliano hayo kabla ya mkataba kuisha.

Hayo yamesemwa leo Mei 27 bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga wakati akijibu swali la Mbunge Jesca Kishoa aliyetaka kujua makubaliano ya mkataba ujao kati ya SONGAS na Serikali yamefikia hatua gani ikiwa mkataba wa awali upo katika mwaka wa mwisho.

Naibu Waziri Kapinga amesema kuwa Serikali itahakikisha maslahi ya Taifa yanazingatiwa kabla ya makubaliano yatakayofuata.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here