Home BIASHARA SEKTA YA UWEKEZAJI NCHINI INAZIDI KUIMARIKA -PROFESA KITILA.

SEKTA YA UWEKEZAJI NCHINI INAZIDI KUIMARIKA -PROFESA KITILA.

Na Esther Mnyika @Lajiji Digital

WAZIRI wa Ofisi ya Rais Uwekezaji na Mipango Profesa Kitila Mkumbo amesema kwa Sekta ya Uwekezaji nchini inazidi kuimarika inayofanya kukua kwa maendeleo ya Uchumi.

Profesa Kitila ameyasema hayo Mei 25 wakati wa hafla ya uzinduzi muunganiko wa kampuni ya Bia ya Heaken na kampuni ya Namibia na kuwa Heaken Beverage itahusishwa vinywaji vya Vileo zaidi ya viwili katika hafla hiyo iliyofanyika Serena Hoteli jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa kampuni hiyo ilikuwa inatoa mapato ya kodi ya shilingi bilioni 11 sasa wanakwenda kutoa mapato ya kodi ya shilingi bilioni 21.

“Sekta ya uwekezaji inkua inakwenda sambasamba na kuongezeka kwa ajira nchini pamoja na biashara.Serikali imeweka mikakati ya kuvutia uwekezaji na ndio inafanya kampuni za nje kuungana na kampuni zilizopo nchini kwetu kutokana na kuwa mazingira mazuri ya uwekezaji na biashara,”amesema Profesa Kitila.

Amesema Serikali ya Awamu ya Sita imeweka mikakati ya Uwekezaji ikiwa ni pamoja wadau wote wanaohusika na uwekezaji kuwa na sauti moja kwenye eneo kuondoa changamoto kwa wanaotaka kuwekeza nchini.

Profesa Kitila amesema kuwa nchi inakwenda kasi katika Uwekezaji ni pamoja na kuwa na rasilimali watu ya kutosha ambao wanaweza kufanya maeneo mbalimbali.

“Nimefurahi kushuhudia uzinduzi wa ofisi mpya ya Heineken nchini Tanzania ukio hili linaashiria hatua muhimu katika kuimarisha mazingira ya uwekezaji
wa Tanzania na kuchangia ukuaji wa uchumi wetu na kuongeza ajira.

” Kujikita kwa Heineken kwenye soko letu ni dhahiri, na ninatazamia kuona matokeo chanya ya jalada lao jipya iliyopanuliwa kwa uchumi na watu wetu,” amesema

Naye Meneja Mkazi wa Kampuni ya HEINEKEN nchini, Obabiyi Fagade, amesema kuunganishwa huku kwa biashara yao hadi kufikia zaidi ya bia ni hatua muhimu katika ukuaji wa kampuni yao nchini Tanzania na ni kielelezo cha imani yao kama Heineken katika ukuaji wa uchumi na maendeleo nchini.

Amesema umiliki wa aina mbalimbali za chapa zinazojulikana imewawezesha kutoa jalada kamili la vinywaji ili kukidhi mahitaji yawatumiaji yanayoendeleza kwa upanuzi wa kinywaji cha Heineken zaidi ya kinywaji cha bia na kuongeza ari yao kutokana na uzoefu wa kipekee kuhudumia watumiaji wa Kitanzania ili kukidhi mahitaji tofauti ya watumiaji wakidumisha nyakati za umoja wa kweli.

” Sasa kuna toleo la kinywaji cha Heineken kwa ajili yako kwa chochote unachohitaji. Uzinduzi huu unaashiria sura ya kuvutia kwetu tunapoendelea kukua na kukidhi soko la Tanzania,” amesema.

Kwa upande wake Meneja wa Masoko na Biashara Lilian Pascal amesema wanakwenda kuongeza ajira na ulipaji kodi kwani idadi iliyokuwepo ilikuwa ya kinywaji kimoja sasa iko zaidi vinywaji viwili.

Amesema Heineken imepanua wigo zaidi kwa kuzindua bidhaa zake mpya mbalimbali kwenye orodha ya jadala lake nchini Tanzania.

Kampuni inayoongoza duniani ya vinywaji,Heineken imesherehekea upanuzi wake zaidi wa vinywaji na kutangaza bidhaa mpya ikionyesha orodha za aina mbalimbali za chapa zilizoanzishwa nchini Tanzania.

Matokeo ya uzinduzi wa bidhaa mbalimbali za vinywaji ni baada ya kukamilika kwa ununuzi wa kampuni ya Distell Group Holdings Limited
(Distell’) na Namibia Breweries Limited (NBL).

Uzinduzi wa biashara mpya ya Heineken pamoja na bidhaa mpya zinazopatikana nchini Tanzania ni hatua muhimu kwa Heineken Beverages International ni sehemu ya mipango yake kupanua biashara na uwekezaji wa kimkakati Heineken inatoa shukrani zake kwa wageni, washirika, na wafuasi wote kwa kujumuika kwa matazamio safari ya kusisimua mbeleni.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here