Home MICHEZO JAMII YAKUMBUSHWA UMUHIMU WA KUSHIRIKI KUFANYA MAZOEZI KUEPUKA MAGONJWA YASIYO YA KUAMBUKIZA

JAMII YAKUMBUSHWA UMUHIMU WA KUSHIRIKI KUFANYA MAZOEZI KUEPUKA MAGONJWA YASIYO YA KUAMBUKIZA

Na Shomari Binda-Musoma

JAMII imeshauriwa kufanya mazoezi ili kuweza kuepukana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa club ya mazoezi ya Musoma Jogging Beda Nyaisa alipokuwa akizungumza na jumuiya ya wafanya mazoezi wa club hiyo.

Amesema mazoezi yana umuhimu mkubwa kiafya na hata madaktari wamekuwa wakihimiza kufanya mazoezi walau dakika 30.

Nyaisa amesema kila mmoja akizingatia kufanya mazoezi kama inavyoelekezwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza yatapungua na hata kumalizika.

Amesema club hiyo imekuwa ikifanya mazoezi zaidi ya miaka 3 na washiriki wote hawana changamoto za kiafya.

” Tunahamasisha jamii kushiriki kufanya mazoezi kutokana na umuhimu wake kiafya na kuendelea kufanya shughuli za kulijenga taifa.

” Hakuna gharama ya kujiunga na club yetu zaidi ya kuja na kuzingatia nidhamu maana hapa tunakutana watu wa tofauti”,amesema Nyaisa.

Katibu wa Musoma Jogging Daud Yunge amesema wanawakaribisha watu mbalimbali kujiunga na kufanya mazoezi.

Mmoja wa washiriki wa club hiyo mzee Salum Hussen amesema anashiriki na vijana kufanya mazoezi na afya yake ipo sawa muda wote

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here