Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi MDk.Hussein Ali Mwinyi leo Mei 26 amemuapisha Sharrif Ali Sharrif kuwa mjumbe wa Tume ya Mipango ya Zanzibar
Hafla hio ya kiapo imefanyika Ikulu Zanzibar kabla ya kuanza kwa Kikao cha Tume hio ya Mipango ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Sharrif Ali Sharrif ni mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na ni Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji wa SMZ.