Home KITAIFA WAZIRI MAKAMBA AMESEMA RAIS DK.SAMIA AMETANGAZA DIPLOMASIA MARA DUFU

WAZIRI MAKAMBA AMESEMA RAIS DK.SAMIA AMETANGAZA DIPLOMASIA MARA DUFU

Na Mwandishi wetu

WAziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki , January Makamba amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amefanya mambo makubwa katika miaka mitatu ya uongozi wake katika kuitangaza nchi kidiplomasia.

Akizungumza leo Machi 20 jijini Dar es Salaam wakati wa Uzinduzi wa Kamati ya kupitia majukumu na maboresho ya kituo cha Uhusiano wa kimataifa cha Dk. Salim Ahmed Salim amesema mafanikio hayo ni pamoja na kuongezeka wa idadi ya wageni kutoka nje kuja Tanzania

Amesema mialiko na mikutano ambayo Rais amealikwa na kushiriki na makubaliano yaliyofikiwa wakati wa ziara alizofanya na viongozi wengine wa Serikali duniani.

“Ukiona kiongozi sauti yake inatafutwa kwenye mambo muhimu ujue yeye mwenyewe na nchi hiyo ina ushawishi inawezekana katika mabadiliko ya Tabianchi, masuala ya rasilimali watu , kilimo, na masuala yote makubwa duniani,”amesema Makamba.

Amesema jambo kubwa kama nchi inalitafuta katika diplomasia ni ushawishi katika jitihada zinazofanyika ni kuongeza ushawishi ili kuweza kupata misaada ,wawekezaji kuja kuwekeza ,ushawishi ili misimamo na mitazamo na kuhusu masuala mbalimbali ubebe uhusika.

Ameeleza kuwa ushahidi wa hivi karibuni Rais alipokuwa Zanzibar viongozi wawili wakubwa wa Afrika mashariki walikwenda kumuona Dk. Samia na kuzungumza naye kutokana na ushawishi wake na kusikia mawazo yake , kumuomba msaada kushauriana nae.

Ameongeza kiwango cha uwekezaji mtaji mwaka 2020 iliyowekezwa nchini ulikuwa wenye thamani ya Dola za Marekani Bilioni moja, mwaka 2023 mtaji uliongizwa nchini ulikuwa ni Dola za Marekani Bilioni tano, hiyo ni jitihada za Rais Samia kutokana na ushawishi wake wa kuweka sera za kiuchumi, ambazo zinavutia uwekezaji .

Amesema lengo la kuzinduliwa kamati hiyo ni kufanya mambo mbali mbali ikiwemo kupendekeza mafunzo na mitaala na kuona namna ya kituo kujenga dhima bora ya fikra.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya kituo cha Dk. Salim Ahmed Salim, Balozi Khamis Kagasheki amesema ni kweli katika miaka mitatu kuna mambo mengi yaliyofanyika Tanzania imekuwa na mahusiano mazuri na mataifa mengine.

Amewaahidi kamati hiyo watajadili na kuona namna ya kufanya kazi zao ili kuona kuna haja ya kutazama chuo hicho kurudi katika hali yake .

kamati hiyo inawajumbe nane na inaongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya kituo cha Dk. Salim Ahmed Salim Balozi Khamis Kagasheki .

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here